Air Niugini: Yakosa mwelekeo na kuanguka katika bahari ya kisiwa cha Weno Micronasia
Air Niugini: Yakosa mwelekeo na kuanguka katika bahari ya kisiwa cha Weno Micronasia
![Maboti madogo madogo yaizunguka ndege ya Air naguini katika maji.](https://ichef.bbci.co.uk/news/768/cpsprodpb/4B6F/production/_103611391_mediaitem103609882.jpg)
Ndege ya abiria imeanguka baharini baada ya kukosa barabara ya ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chuuk International huko Micronesiam kulingana na maafisa wa uwanja huo wa ndege.
Ndege hiyo kutoka kampuni ya ndege ya Air Niugini kutoka taifa la Papua New Guinea ilionekana ndani ya maji ya kina kifupi karibu na pwani ya eneo hilo.
Wakaazi wa eneo hilo walichukua hatua ya haraka kupitia kuifuata ndege hiyo wakiwa wameabiri maboti na kuweza kuwasaidia abiria wake 36 pamoja na wafanyika zi 11.
- Ni kwanini watoto walemavu wanauawa Kenya?
- Je Patrick Mfugale ni nani?
- Uzinduzi wa Daraja la juu la Mfugale Tanzania
Afisa mmoja wa hospitali aliambia chombo cha habari cha reuters kwamba abiria wanne walijeruhiwa vibaya baada ya ajali hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa ikipaa kutoka kisiwa cha Pohnpei huko Micronasia kuelekea bandari ya Moresby, mji mkuu wa Papua New Guinea , huku ikitarajiwa kusimama katika kisiwa cha Micronasia cha Weno ikiwa safarini.
Kampuni ya Air Naguini imesema kuwa ndege yake aina ya Boeing 737-800 iliokosa barabara yake na kuanguka kando kutokana na hali mbaya ya hewa iliosababishwa na mbvua kubwa.
Uchunguzi unatarajiwa kuanza , maafisa wa uwanja huo wa ndege wamesema.
![Ndewge ya Air Niugini ikiwa ndani ya maji ya Weno, Chuuk, Micronesia](https://ichef.bbci.co.uk/news/768/cpsprodpb/E7AF/production/_103611395_mediaitem103611394.jpg)
![watu waliokuwa katika maboti madogo waizunguka ndege hiyo](https://ichef.bbci.co.uk/news/768/cpsprodpb/183EF/production/_103611399_mediaitem103611398.jpg)
![Ndege ya Air Niugini ikiwa majini huko Weno, Chuuk, Micronesia](https://ichef.bbci.co.uk/news/768/cpsprodpb/49CA/production/_103609881_049601333-1.jpg)
"Nilidhani tulishuka vibaya hadi nikaona tundu upande mmoja wa ndege hiyo na majia yakaanz akuingia, Niulisema haifa kuwa hivi, alisema.maji katika chumba cha rubani yalikuwa yamejaa hadi kufikia kiunoni kabla ya waokoaji kuwasili'', aliongezea.
Dkt James Yaingeluo kutoka jimbo la hospitali ya Chuuk ni miongoni mwa watu waliowasili wa kwanza katika eneo la tukio na kuiambia BBC kwamba alikutana na mgogoro.
Muda tu ndege ilipofungua mlango wake, ilikuwa balaa.
Kila mtu alijaribu kutoka kupitia mlango huo, alisema.
Bahati nzuri kulikuwa na mboti takriban 20 katika maji na tulifanikiwa kumuokoa kila mmoja.
![ramani inayoonyesha eneo la Micronesia na Papua New Guinea](https://ichef.bbci.co.uk/news/768/cpsprodpb/D2F1/production/_103610045_plane_crash_papua_new_guinea_v2_map640-nc.png)
![Wakazzi wa eneo hilo wakiikaribia ndege ya Air Niugini katika kisiwa cha Weno, huko Micronesia.](https://ichef.bbci.co.uk/news/768/cpsprodpb/3085/production/_103612421_hi049605060.jpg)
![watu waliokuwa katika maboti madogo waizunguka ndege hiyo](https://ichef.bbci.co.uk/news/768/cpsprodpb/16C89/production/_103612339_hi049602152.jpg)
.
Comments
Post a Comment