Story fupi ya kusisimua.

Nikiwa Mdogo nilikua mkorofi na mtundu sana, nilipenda kupigana na watu na hata watu wakubwa sikuwaogopa maana nilijua mama yangu ananipenda sana na nilikua nikitoka shule alikua ananipaka dawa hata kama nina majeraha

Nilipenda sana uangalifu wa mama na nilifanya kila aina ya utundu, maana nilijua mama yupo na atanitetea kwa chochote kile. Mama alikua anaumia sana na wakati wingne analia kabisa lakini sikujali hill.

Sikumoja bibi yangu aliumwa(mama yake mama) ikabidi mama aende kumuuguza, dah! Kile kipindi kilikua kigumu sana kwangu niliogopa kupigana na hata nikionewa nilibaki natulia tu maana mtetezi hayupo.

Mara nyingi nilikua nikitoka shule naenda barabarani natamani nimwone mama akija wakati mwingine hadi machozi yalinitoka kwa wakati ule nilikonda japo nilikua nikila vizur.

 Sikumoja mama alikuja, kwa kweli nilifurahi sana, nilimumbatia kwa muda mrefu sana lakini mama alikonda pia kwaajili ya hali ngumu ya kijijini kwa bibi.

Mama aliniangalia akaniambia "mwanangu hali yangu ni mbaya nimepata ugonjwa wakati namuuguza bibi yako, nilikua nikiwaza unaishiaje nilikua nikiwaza usalama wako, na baada ya muda niliumwa lakini majibu ya dactari aliniambia nina presha iliyo sababishwa na mawazo. Mwanangu nakiomba badilika presha hii isije ikaniondolea uhai wangu maana sitaki kuondoka na kukuacha mwanangu."

nilikaa nikatafakari kwanini namsababishia mama ugonja, niliona mama akifariki kwaajili ya presha moja kwa moja itakua ni mimi nimemuua. Nililia nikajua ninampenda sana mama nikajihoj mtu ninaye mpenda inanipasa kumsumbua? nikajijibu hapana.

kwa mara ya kwanza niliondoka na kwenda kanisani nilitubu, niliporudi nyumbani nilimuahidi mama kuto muumiza tena kwa hali yoyote ile. Nilifanya uamuzi na nilikua mtoto mzuri. Niliheshimu wakubwa kwa wadogo. Na hapo ndipo nilipoona baraka za Mungu kwangu kwanzia kwenye masomo mpaka Kazi za kawaida.

FUNZO

Kwenye maisha ya kawaida
Watu wengi wamekua na tabia ya kuwatesa wenzio baada ya kujua kuwa wanapendwa, huwa wanapendwa kufanya chochote kile watakacho kwa mtu yule bila kujua mwenzie anachoka kiasi gani na anaumia kiasi gani kwake. Tunapaswa kubadilika kila kitu kwenye maisha yetu tukiheshimu kama ni mtu anakupenda nawe inapaswa kumpenda na kumjali sio kumtesa.


Katika maswala ya imani

Mungu ndie baba na bwana wetu, ndiye aliye tuumba kwa mfano wake. Tulipopotea kwa maasi na dhambi zetu aliona wote tunaangamia kwaajili ya upendo alimtuma mwanae wa pekee Yesu kristo ili atakae mwamini asipotee Bali kuupata uzima wa milele. Lakini sisi wanadamu tumekuwa wagumu sana kuelewa na kusikia hatutaki kuelewa upendo wa bwana tuna ng'ang'ana kumtesa Yesu kila Mara na kila wakati. Tunao Kazi na tunao wajibu wa kubadilika na kurudi na kutubu kwa bwana, na baada ya hapo kushika amri zake hii itaonesha ni jinsi gani tunaujali upendo wake kwa kuheshimu amri zake.

Mungu akubariki na akuongezee miaka ya heri hapa duniani
I love you
Kama umependa Ujumbe huu usisahau kuLIKE NA kuSHARE link hii watu wengi waupate Ujumbe huh.
THANK YOU

Comments

Popular posts from this blog