NJIA KUU ZA KUFIKIA MAFANIKIO

NJIA KUU ZA KUFIKIA MAFANIKIO
Napenda kuwasalimu sana, leo ningependa kuzungumzia kidogo kuhusu njia kuu za kukufikisha kwenye mafanikio, lakini swali ya tote tuangalie mini maana ya mafanikio
           Mafanikio ni hali ya kutoka katika sehemu ya chini( hali duni) ya kimaisha na kufikia hatua uliyokua ukiihitaji au ukiifikiria katika maisha yako. 
Mwingine akasema mafanikio ni hatua ambayo mtu anaifikia na kua amefikia ndoto zake.
Maana zote mbili ni sawa lakini ombi kubwa la watu wengi na haaaa vijana mafanikia, ni kutimiza ndoto zake alizo jiwekea, sasa moja kwa mmoja bila kupoteza muda nizungumzie mini kifanyike ili mtu afikie mafanikio au ndoto alizo nazo
  1. Kumweshimu na kumtumaini Mungu
Kwa hali mmoja au nyingine tunaweza jisifu au kufanya Kazi tukitumainia nguvu zetu mwenyewe na kumsahau aliye tupa uhai, mtu mmoja akasema hivi "vitu vyote humu duniani tunavyovifanya ni 0 lakini Mungu ni 1". Katika maneno hayo unaweza fikiria na kutambua kua unapotanguliza mambo yako na Kazi zako mbele na kumwacha Mungu awe wa mwisho, ina maana hivi kama una mambo matano ndo anafuata Mungu basi ni 000001. Lakini unapokua na mambo hayo hayo matano lakini Mungu wa kwanza inakua hivi 100000. Sasa eb jarib kujifunza kitu katika hayo mambo mawili namba zipi zinathamani?. Utakuja kugundua kua jambo hili, unapo mtanguliza Mungu basi mambo yako yote yanakua na thamani hivyo kabla ya vyote tumtangulize Mungu kwanza.

      2.  Kuwa na juhudi kwa lolote lile utakalokua unalifanya.
. Jiamini
Mafanikio ya kweli yanaanza na wewe. Hivyo, kujiamini ni msingi mzuri utakaokufanya utambue uwezo wako katika kufanya jambo fulani. Amini uwezo wa kufanya jambo hilo uko mikononi mwako. Usijishushe, jipime kwa mengi mazuri unayoweza kufanya, ikatae roho ya kujiona huwezi.


3. Panga na tekeleza kwa vitendo

Kumbuka, ukishindwa kupanga ujue umepanga kushindwa. Kuwa na mipango inayopimika na kutekelezeka kwa kiwango cha juu. Usiwe na mipango tu mikubwa ambayo hata utekelezaji wake hauwezekani. Unapopanga fikiria wapi utapata rasilimali na jinsi ya kutelezeka, lakini pia mpango wako ukupe uwezo wa kuutathmini na kujipima mwisho wa kazi hiyo. Hata hivyo, mipango haitakuwa na maana kama hautaitekeleza kwa ufanisi. Ukishindwa kutekeleza mpango wako, rudi angalia ulipoteleza ili urekebishe na sio kuufuta mpango mzima bila sababu za msingi.


4. Tengeneza mtandao na wasiliana

Mtandao ni kama daraja au miundombinu ya kuyafikia mafanikio. Hakikisha haujifungii kwenye dunia yako peke yako. Hakikisha kila unaekutana naye na kupata nafasi ya kumfahamu kama mtu anayeweza kuwa sehemu ya daraja bora kwa namna moja au nyingine, anakuwa sehemu ya mtandao wako.
Lakini kuwa na mtandao wa watu pekee hautoshi kama hautawasiliana nao. Kuwasiliana na mtandao huo ni kuufanya uwe ‘active’ ili isionekane kama unawatafuta wakati ukiwa na shida tu. Aidha, unapaswa kujipima kwa kuangalia watu wangapi wanakufahamu wewe zaidi ya watu wangapi unaowafahamu. Kwa mfano: wewe unamfahamu Mkurugenzi wa kampuni ‘A’, Jiulize, je, yeye anakufahamu? Kama hakufahamu basi yeye sio sehemu ya mtandao wako.

MENGINEYO MUHIMU SANA

  • Tafuta fulsa kila kona.
  • Tumia kipaji chako.
  • Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.



  • Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.

  • Usipoteze muda - jali muda kuliko kitu chochote kwani muda ndio kila kitu, muda ni mali.
  • Shiriki kwenye makongamano au semina mbalimbali za ujasiriamali.

  • Kuwa na vyanzo vingi vya kukuletea kipato.

  • Tafuta maarifa kwa mamilionea mbalimbali duniani - soma historia za mamilionea jinsi walivyofanikiwa.

  • Jenga urafiki na taasisi za kifedha - mamilionea wengi hukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha - tembelea taasisi za fedha watakupa ushauri mbalimbali na watakupa mkopo, usisikilize maneno ya watu kuwa taasisi za pesa ni za watu matajiri hiyo sio kweli.

  • Kuwa na shauku, kuwa na fikra za kuwa milionea na wewe utakuwa.USIWAZIE KUSHINDWA

  • Kuwa na imani kwamba utakuwa milionea na itakuwa hivyo. KWA KUFANYA. SIO IMAN TU.

  • Wekeza ktk miradi au biashara mbalimbali. USIOGOPE KUTHUBUTU

  • Wekeza sehemu yenye mahitaji ya bidhaa inayotakiwa kuzalishwa - angalia fursa hapo ulipo na wekeza. SIO KUFUJA PESA

  • Kuwa na bajeti katika mapato na matumizi yako. NIDHAMU MUHIMU KATIKA PESA

  • Kuwa na wazo (Business idea): mamilionea wengi hutumia mawazo kutoka kwa watu mbalimbali kutengeneza pesa. Wazo ndio cheti cha kuwa milionea anza sasa fanyia kazi wazo lako ili kukuletea fedha.

  • Fanya vitu wewe mwenyewe - acha kufanya vitu kama fulani, usiige mtu, buni vya kwako, mamilionea huwa hawaigi, ukiwa mkweli kwako utakuwa mkweli kwa watu

  • Kuwa na malengo - kumbuka hakuna maendeleo pasipo na malengo, fahamu hilo.,, PLANS AND SELF COMMITMENT

  • Kuwa na moyo wa ujasiri - usiogope kushindwa jitahidi ktk kupambana na maisha usikubali kubezwa au kuvunjwa moyo. Ukianguka nyanyuka tena, usifikirie kutakuwa na mtu wa kukusaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe.UKIANGUKA USIOGOPE KUINUKA

  • Kuwa karibu na matajiri -usiogope kwani hao ni binadamu kama wewe, jaribu kuwadadisi ili wakupe mbinu mbali za kuwa tajiri hadi milionea. Ukiwa karibu nao unaweza ukapata nafasi ya kazi au kukuunganishia biashara ukaanza kufanya na kufanikiwa.

  • Fanya vitu kitofauti; fanya vitu vigeni, muonekano tofauti ingawa biashara ni ile ile, tumia lugha tofauti, panga bei tofauti, nk. Mfano aina tofauti za simenti, chupa za soda na juisi nk.

  • Kuwa na mtazamo chanya - usikubali mawazo hasi, marafiki zako wawe na mawazo chanya, usikubali kuvunjika moyo na usikubali mawazo yako yaingiliwe na mtu.
  • Anza kufanyia kazi wazo lako usisubiri mtu.

  • Kuwa na mipaka katika mambo yako - usifanye mambo kwa mkumbo, usiige, buni mambo yako. Mamilionea wengi wanabuni mambo yao hawapangiwi na mtu

  • Kuwa mwaminifu -mamilionea wengi ni waaminifu ktk mali za watu. Wengi walikuwa wakipewa mali wakauze ndio walipe pesa, wanadhaminiwa malighafi za viwandani hadi wanamiliki viwanda vyao. Uaminifu ndio njia ya kukufanya uwe milionea.

  • Pokea ushauri kwa watu hasa kuhusiana na biashara yako - waulize watu kuhusu huduma yako ya biashara wanaionaje na fanyia kazi ushauri wao.
  • Kuwa na plani katika kazi zako kila siku.

  • Kuwa na maono ya jinsi unavyotaka maisha yako yawe

  • Panua soko la bidhaa zako usitegemee soko la sehemu moja

  • Ubunifu ni muhimu sana - fanya ubunifu ktk kuuza bidhaa zako ili mauzo yasishuke, kuwa mbunifu ktk wateja wako kwani itakusaidia kugundua wateja wako wanataka nini - kuwa karibu nao, wasikilize, waheshimu nk.

  • Kuwa milionea kunaanzia kichwani mwako-ukiweka mawazo yako kichwani utakuwa milionea kweli utakuwa sio kusema tu mdomoni. Amini utakuwa milionea na utakuwa kweli

  • PIGA KAZI

  • Maneno ya walioshindwa yasikukwamishe safari yako ya kuwa milionea

  • Ondoa neno haiwezekani wewe kuwa milionea - kila binadamu anaweza kuwa milionea

  • Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa - kumbuka neema ya Mungu ndio imekufikisha hapo ulipo hivyo toa msaada kwa watu wasiojiweza, yatima, masikini, wajane, wagonjwa, toa sadaka, walemavu nk



Comments

Popular posts from this blog