MZEE MAJUTO; HABARI ZA HIVI PUNDE.. Amri Athuman (king MAJUTO) afariki dunia

R.I.P KING MAJUTO( Amri At human)

aliekua msanii maarufu na mchekeshaji ( bongo movie) amefariki katika hospital ya Muhimbili leo saa mbili usiku
Chanzo cha habari EATV


Chanzo kingine



Breaking News: Mzee King Majuto Afariki Dunia



MSANII nguli wa vichekesho Tanzania, Amri Athuman ‘Mzee King Majuto’ amefariki dunia majira ya saa 2:00 usiku huu wa Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa.
Mtoto wa marehemu aitwaye Abuu amethibitisha kifo cha baba yake.
Pia, mchekeshaji Joti ndio wa kwanza kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa instagram.
“R.I.P King Majuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana katika Tasnia ya Comedy Tanzania, sisi wanao, tutakukumbuka kwa kazi zako, upendo wako, tabasamu lako Daima milele, tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi, pumzika kwa Amani Mzee wetu,” amendika Joti.
Mzee Majuto alizaliwa mwaka 1948 mkoani Tanga na kusoma Shule Msambwini, mkoani humo, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 10.
Hivi karibuni Mzee Majuto alisafirishwa na kupelekwa nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejea nchini ambapo alipelekwa Muhimbili kuendelea na tiba yake.
Mzee Majuto ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC), alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.

Comments

Popular posts from this blog