KOMBE LA DUNIA LEO
Kombe la Dunia 2018 - mambo muhimu kuhusu nchi ambazo tayari zimefuzu michuano ya Urusi
![Neymar](https://ichef.bbci.co.uk/news/768/cpsprodpb/4457/production/_97659471_brazil_gety.jpg)
Michuano ya mwisho ya hatua za makundi kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka ujao inaendelea kufanyika. Kwa sasa mataifa 22 tayari yamejikatia tiketi kushiriki michuano hiyo itakayoshirikisha nchi 32 mwaka ujao.
Mabingwa mara tano Brazil wamefuzu, sawa na mabingwa watetezi Ujerumani,pamoja na Argentina, Iceland, Ubelgiji, Colombia, Costa Rica, England, Misri, Iran, Japan, Mexico, Nigeria, Panama, Poland, Saudi Arabia,Serbia, KoreaKusini, Ufaransa, Ureno, Uhispaniana Uruguay.
Walifikaje huko? Nani wachezaji wao nyota? Na wakufunzi waliowafikisha huko?
ULAYA
Urusi (wenyeji)
Ustadi: Vijana hao chini ya Stanislav Cherchesov watakiwa timu ya nne kutoka Urusi kucheza Kombe la Dunia. Mara ya kwanza walishiriki Marekani '94 - ingawa Muungano wa Usovieti ulimaliza nambari nne mwaka 1966.
Ndio wenyeji |
---|
Kikosi chote cha wachezaji wa Urusi waliocheza Kombe la Mabara mwaka 2017 Urusi walikuwa wanachezea klabu za nyumbani |
Mchezaji nyota: Kipa wao mkongwe Igor Akinfeev amechezea nchi hiyo zaidi ya mechi 100 na uzoefu wake utakwua muhimu.
Akinfeev, 31, amechezea CSKA Moscow maisha yake yote ya uchezaji soka ya kulipwa. Huenda akawa nahodha wa Urusi.
Wachezaji Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja.
Mkufunzi? Cherchesov ni kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Muungano wa Usovieti na Urusi. Lengo lake ni kuwafikisha nusu fainali.
Ubelgiji
Ustadi: Hawakufuzu kwa michuano miwili iliyotangulia lakini Brazil 2014 walifika robofainali, ambapo waliondolewa na Argentina. Mwaka 1986 walimaliza wa nne.
![Eden Hazard](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/9277/production/_97659473_hazard_getty.jpg)
Mchezaji nyota: Eden Hazard ambaye pia ndiye nahodha
Wachezaji Ligi ya Premia: Michy Batshuayi, Thibaut Courtois, Eden Hazard (wote wa Chelsea), Simon Mignolet (Liverpool), Toby Alderweireld, Moussa Dembele, Jan Vertonghen, (wote wa Tottenham), Kevin de Bruyne, Vincent Kompany (wa Manchester City), Marouane Fellaini, Romelu Lukaku (wa Manchester United), Steven Defour (Burnley), Nacer Chadli (West Brom), Kevin Mirallas (Everton), Christian Benteke (Crystal Palace), Divock Origi (Wolfsburg, kwa mkopo kutoka Liverpool), Christian Kabasele (Watford).
Mkufunzi? Roberto Martinez aliyesaidia Wigan kushinda Kombe la FA mwaka 2013
England
Ustadi: Tangu waliposhinda Kombe la Dunia 1966, England wamefika nusu fainali mara moja pekee - mwaka 1990, ambapo walimaliza wa nne. Miaka minne iliyopita, waliondolewa hatua ya makundi. Ilikuwa mara yao ya mwisho kukosa kupita hatua ya makundi tangu 1958.
![England failed to progress from the group stages of the World Cup in 2014](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/10F82/production/_98160596_gettyimages-451159758.jpg)
Mchezaji nyota: Harry Kane amefunga magoli 13 akichezea klabu ya taifa Septemba na kwa sasa ni miongoni mwa washambuliaji wanaofunga mabao sana. Mwaka 2017 amefunga mabao 27 ambapo amepitwa tu na Lionel Messi, anayemzidi kwa magoli tisa.
Wachezaji Ligi ya Premia: Kikosi chote cha England hucheza EPL
Mkufunzi? Gareth Southgate anaongoza timu kwa mara ya kwanza katika michuano mikubwa.
Ufaransa
Ustadi: Ufaransa walishinda Kombe la Dunia walipokuwa wenyeji wa michuano hiyo 1998 na walifika fainali miaka minane iliyofuata ambapo walishindwa na Italia. Walifika robofainali Brazil 2014. Walimaliza wa pili Euro 2016.
![Antoine Griezmann](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/167CA/production/_98260129_antoine_griezmann.jpg)
Mchezaji nyota: Antoine Griezmann. Mshambuliaji huyu wa Atletico Madrid alikuwa mfungaji bora wa Ufaransa ambapo aliwafungia mabao sita na kuwawezesha kufika fainali Euro 2016.
Alifunga bao la pili kuwawezesha kulaza Belarus 2-1 na kufuzu 10 Oktoba.
Wachezaji wa Ligi ya Premia: Laurent Koscielny, Alexandre Lacazette and Olivier Giroud (wote wa Arsenal), Tiemoue Bakayoko na N'Golo Kante (wote wawili Chelsea), Yohan Cabaye (Crystal Palace), Eliaquim Mangala na Benjamin Mendy (wote wawili Manchester City), Anthony Martial na Paul Pogba (wote wawili Manchester United), Kurt Zouma (Stoke, kwa mkopo kutoka Chelsea), Hugo Lloris na Moussa Sissoko (wote wawili Tottenham).
Mkufunzi wao? Didier Deschamps alichezea Ufaransa mechi 103 na aliwasaidia kushinda Kombe la Dunia 1998 na ubingwa wa Ulaya 2000. Amekuwa mkufunzi wao tangu Julai 2012. Aliwafikisha fainali Euro 2016, aambapo walilazwa na Ureno 1-0.
Ujerumani
Ustadi: Ni mabingwa watetezi, wameshinda Kombe la Dunia mara nne na wameorodheshwa kuwa timu bora zaidi duniani na Fifa kwa sasa.
![Toni Kroos has scored 12 goals in 78 appearances for Germany](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/CF36/production/_98164035_gettyimages-842661340.jpg)
Mchezaji nyota: Toni Kroos. Kando na Thomas Muller na Mesut Ozil, kiungo huyo wa Real Madrid ndiye mchezaji mzoefu zaidi kwenye kikosi.
Alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Dunia 2014, ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili, La Liga mara moja na Kombe la Dunia la Klabu mara mbili.
Wachezaji Ligi ya Premia: Shkodran Mustafi (Arsenal), Antonio Rudiger (Chelsea), Emre Can (Liverpool), Ilkay Gundogan (Manchester City), Mesut Ozil (Arsenal), Leroy Sane (Manchester City).
Meneja? Joachim Low. Alikuwa mkufunzi msaidizi wa Jurgen Klinsmann 2004 hadi 2006, alipochukua hatamu. Aliwaongoza kushinda Kombe la Dunia mwaka 2014 na pia alishinda Kombe la Mabara mwaka huu. Hata hivyo hajashinda Euro. Walimaliza wa pili mwaka 2008 na nafasi ya tatu 2012.
Iceland
Ustadi: Iceland watakuwa wanashiriki Kombe la Dunia wka mara ya kwanza kabisa baada ya ushindi wao dhidi ya Kosovo tarehe 9 Oktoba kuwahakikishia nafasi.
Wamekuwa wakifanikiwa sana karibuni. Walifika Euro 2016, na kulaza England raundi ya pili kabla ya kulazwa 5-2 na wenyeji katika robofainali.
Mchezaji muhimu: Ni vigumu kumtazama mchezaji mwingine ila Gylfi Sigurdsson wa Everton. Mchezaji huyo wa miaka 28 aliwafungia bao la kwanza dhidi ya Kosovo na ni mshambuliaji hatari sana, hasa kwa makombora ya mbali.
![Gylfi Sigurdsson celebrates an Iceland goal on the night they secured qualification](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/11E1C/production/_98244237_sigurdssongetty.jpg)
Wachezaji wa Ligi ya PremiaGylfi Sigurdsson (Everton), Johann Berg Gudmundsson (Burnley).
Wachezaji Championship: Birkir Bjarnason (Aston Villa), Horour Bjorgvin Magnusson (Bristol City), Jon Dadi Bodvarsson (Reading).
Mkufunzi? Heimir Hallgrimsson, 50, ni daktari wa meno aliyekuwa anasimamia timu hiyo kwa pamoja na Lars Largerback wa Sweden wakati wa michuano ya ubingwa Ulaya nchini Ufaransa. Hallgrimsson alichukua usukani kamili baada ya Euro 2016 na kuwasaidia kufana mechi za kufuzu.
Poland
Ustadi: Poland wameorodheshwa wa sita duniani. Hawajawahi kushinda Kombe la Dunia lakini mwaka huu wanaamini wana kikosi stadi zaidi. Ufanisi wao awali ulikuwa kumaliza nafasi ya tatu, mwaka 1974 na 1982.
![Bayern Munich forward Robert Lewandowsk](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/2522/production/_98160590_lewandowski2.jpg)
Mchezaji nyota: Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski amefunga mabao 16 katika mechi tisa za kufuzu Kombe la Dunia akiwa na Poland. Anashikilia nafasi ya tatu kufunga mabao mengi historia ya Poland. Ndiye nahodha na amefunga mabao 51 mechi 91 za kimataifa.
Wachezaji Ligi ya Premia: Lukasz Fabianski (Swansea), Grzegorz Krychowiak (West Bromwich Albion), Kamil Grosicki (Hull City)
Wachezaji Championship: Pawel Wszolek (Queens Park Rangers)
Mkufunzi? Adam Nawalka amewaongoza tangu Novemba 2013 mechi 39. Mkataba wake unafika mwisho Desemba lakini aliwafikisha robo fainali Euro 2016, miaka miwili baada yao kushindwa kufuzu Kombe la Dunia 2014.
Ureno
Ustadi: Ndio mabingwa wa sasa wa Ulaya, ambapo walilaza Ufaransa 1-0 fainali. Ufanisi wao zaidi Kombe la Dunia ulikuwa walipomaliza wa tatu mwaka 1996. Walifika pia nusufainali 2006 lakini Brazil 2014 waliondolewa hatua ya makundi.
![Cristiano Ronaldo](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/28A6/production/_98260401_cristiano_ronaldo.jpg)
Mchezaji tegemeo: Nani mwingine? Cristiano Ronaldo. Ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani mara nne, na amechezea taifa lake mechi nyingi zaidi. Aidha, anashikilia rekodi ya ufungaji timu yake ya taifa. Ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara nne.
Alifunga mabao 15 akichezea Ureno mechi za kufuzu Kombe la Dunia.
Wachezaji Ligi ya Premia: Adrien Silva (Leicester), Bernardo Silva (Manchester City), Cedric Soares (Southampton), Renato Sanches (Swansea, kwa mkopo kutoka Bayern Munich), Jose Fonte (West Ham).
Mchezaji wa Championship: Nelson Oliveira (Norwich)
Mchezaji Ligi Kuu ya Scotland: Bruno Alves (Rangers)
Meneja? Fernando Santos alichukua hatamu Septemba 2014 na kuwaongoza kushinda Euro mara ya kwanza 2016. Alikuwa pia meneja wa Ugiriki Kombe la Dunia 2014 ambapo aliwafikisha hatua ya 16 bora lakini wakashindwa na Costa Rica.
Serbia
Ustadi: Mwaka ujao itakuwa mara ya 12 kwa Serbia kucheza Kombe la Dunia. Hawakufanikiwa kupita hatua ya makundi mwaka 2006 na 2010.
![Branislav Ivanovic amechezea Serbia mechi 95](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/1498F/production/_98176348_gettyimages-613645202.jpg)
Mchezaji nyota: Branislav Ivanovic anakaribia kuchezea taifa lake mechi 100 na ni mchezaji muhimu sana kwao. Ndiye nahodha na kiongozi.
Wachezaji Ligi ya Premia: Nemanja Matic (Manchester United), Aleksandar Mitrovic (Newcastle), Lazar Markovic (Liverpool), Dusan Tadic (Southampton).
Mkufunzi? Slavoljub Muslin, aliyeteuliwa Mei 2016, ni mkufunzi ambaye amesafiri kwingi. Anafanya kazi ya kuwa mkufunzi wa timu ya taifa mara ya kwanza na hajawahi kuongoza timu katika michuano mikubwa. Lakini amefanikiwa ligini Bulgaria.
Uhispania
Ustadi: Wameorodheshwa 11 duniani. Walikuwa namba moja duniani kuanzia 2008 hadi 2013.
Walikuwa mabingwa wa dunia 2010 na mabingwa wa Ulaya 2008 na 2012.
![Isco scored two goals in Spain's 3-0 win over Italy in February](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/B6A5/production/_98175764_gettyimages-845896788.jpg)
Mchezaji nyota: Kiungo wa kati mshambululiaji wa Real Madrid Isco amekuwa kwenye fomu nzuri sana mechi za kufuzu. Amefunga mabao sita mechi saba za karibuni zaidi za Uhispania. Amefunga mabao saba mechi 23 za kimataifa.
Wachezaji Ligi ya Premia: Juan Mata (Manchester United), Nacho Monreal (Arsenal), Alvaro Morata (Chelsea), David de Gea (Manchester United), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Ander Herrera (Manchester United), Pedro (Chelsea), David Silva (Manchester City).
Mkufunzi? Julen Lopetegui aliteuliwa Julai 2016 na hajashindwa mechi 13 ambazo amewaongoza.
AMERIKA KUSINI
Brazil
Ustadi: Washindi mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002, Brazil walilazwa 7-1 hatua ya makundi na Ujerumamni mwaka 2014.
![Neymar](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/4457/production/_97659471_brazil_gety.jpg)
Mchezaji nyota: Neymar. Alinunuliwa £200m na Paris St-Germain na amekuwa akifunga bao na kusaidia kila mechi tangu wakati huo. Pele amesema Neymar, 25, ndiye mchezaji bora zaidi wa taifa hilo na anaamini atashinda Ballon d'Or.
Wachezaji Ligi ya Premia: Ederson, Fernandinho, Gabriel Jesus (wote wa Manchester City), Philippe Coutinho, Roberto Firmino (wa Liverpool), Willian (Chelsea).
Mkufunzi? Tite alichukua nafasi ya Dunga wakiwa nafasi ya sita, theluthi ya mechi za kufuzu zikiwa zimechezwa. Lakini mkufunzi huyo wa zamani wa Corinthians, 56, amewasaidia kuwa alama 11 mbele ya Colombia kileleni zikiwa zimesalia mechi tatu.
Argentina
Ustadi: Argentina wameshinda Kombe la Dunia mara mbili - 1978 na 1986 - na wamemaliza wa pili mara tatu mwaka 1930, 1990 na nchini Brazil 2014, ambapo walishindwa 1-0 na Ujerumani fainali.
![Lionel Messi](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/B870/production/_98261274_messi_goal2.jpg)
Mchezaji nyota: Lionel Messi. Messi, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani mara nne na alifunga hat-trick mechi za kufuzu dhidi ya Ecuador kuwafikisha Argentina michuano hiyo ya Urusi.
Wachezaji wa ligi ya premia: Sergio Aguero na Nicolas Otamendi (wote wawili Manchester City), Sergio Romero (Manchester United), Manuel Lanzini (West Ham).
Meneja: Meneja wa zamani wa Chile Jorge Sampaoli, aliyeongoza Chile Copa America mwaka 2015, aliteuliwa meneja wa Argentina Mei 2017. Alifanikiwa kibarua chake cha kwanza, kuhakikisha wanafuzu kwa Kombe la Dunia.
Colombia
Ustadi: Colombia walifanikiwa zaidi Brazil 2014 walipofika robofainali lakini wakashindwa 2-1 na Brazil.
![James Rodriguez](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/6A50/production/_98261272_rodriguez.jpg)
Mchezaji nyota: James Rodriguez. Mshambuliaji kiungo wa kati aliye Bayern Munich kwa mkopo kutoka Real Madrid, alishinda tuzo ya Kiatu cha Dhahabu kwa ufungaji mabao mengi zaidi Kombe la Dunia 2014. Alifunga mabao sita michuano hiyo.
Wachezaji wa Ligi ya Premia: David Ospina (Arsenal), Jose Izquierdo (Brighton), Davinson Sanchez (Tottenham)
Meneja: Jose Pekerman ameongoza Colombia tangu 2012 na alishinda tuzo ya Kocha wa Mwaka Amerika Kusini mara tatu tangu wakati huo.
Uruguay
Ustadi: Uruguay walishinda Kombe la Dunia mara ya kwanza 1930 kisha tena 1950 lakini walifika hatua ya 16 bora pekee Brazil 2014.
![Luis Suarez](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/10690/production/_98261276_luis_suarez.jpg)
Mchezaji nyota: Luis Suarez. Nyota huyu wa Barcelona ndiye mfungaji mabao bora zaidi wa uruguay na alifunga mawili mechi yao ya mwisho ya kufuzu dhidi ya Bolivia.
Mchezaji wa Championship: Abel Hernandez (Hull)
Meneja: Oscar Tabarez amekuwa kwenye usukani Uruguay tangu 2006 na kuwaongoza kushinda Copa America mwaka 2011.
AMERIKA KASKAZINI NA KATI na CARIBBEAN
Mexico
Ustadi: Mexico wamefika hatua ya muondoano kila michuano ya Kombe la Dunia sita iliyochezwa. Walifika robofainali wakiwa wenyeji mwaka 1986.
Mchezaji nyota: Hirving Lozano amefunga mabao matatu mechi tatu kati aihame Pachuca na kwenda PSV Eindhoven majira ya joto.
Lozano, 22, ameanza kuwa nyota timu ya taifa ambapo alifunga bao la ushindi dhidi ya Panama.
Alimpendeza hata Diego Maradona akicheza mechi yake ya kwanza Eredivisie.
Wachezaji Ligi ya Premia: Javier Hernandez (West Ham).
Mkufunzi? Meneja msaidizi wa zamani waManchester City Juan Carlos Osorio ndiye anayewaongoza. Alikuwa awali amepigwa marufuku mechi sita na Fifa kwa kumtusi mwamuzi Kombe la Mabara. Ni raia wa Colombia aliyesomea stashahada ya sayansi na soka kutoka chuo kikuu cha John Moores cha Liverpool.
Costa Rica
Ustadi: Urusi 2018 itakuwa mara ya tano kwa Los Ticos kucheza michuano ya Kombe la Dunia.
Brazil walimaliza kileleni mwa kundi lililokuwa na Uruguay, Italia, na England. Waliondolewa robofainali kwa mikwaju ya penalti na Uholanzi.
Mchezaji nyota: Beki wa Bologna Giancarlo Gonzalez alikuwa kwenye kikosi bora cha wachanganuzi wa BBC wa Kombe la Dunia mwaka 2014 lakini ufanisi wa sasa wa Costa Rica unatokana na kipa Keylor Navas, 30. Alicheza vyema sana 2014 kiasi cha Real Madrid kumnunua na sasa ndiye kipa wao nambari wani.
Ameshinda La Liga na makombe mawili ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
![Costa Rica keeper Keylor Navas](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/10D3A/production/_98222986_navas_getty.jpg)
Wachezaji Ligi ya Premia: Joel Campbell wa Arsenal ambaye yuko kwa mkopo Real Betis.
Mkufunzi? Oscar Ramirez ambaye alikuwa mchezaji Costa Rica walipocheza Kombe la Dunia mara ya kwanza 1990. Alichukua usukani 2015 baada ya Paulo Wanchope kujiuzulu.
Panama
Ustadi: Ni mara yao ya kwanza kufika Kombe la Dunia baada ya ushindi wao dhidi ya Costa Rica mechi yao ya mwisho. Walimaliza wa pili Kombe la Dhahabu la Concacaf mwaka 2013.
Mchezaji nyota: Luis Tejada. Ana miaka 35 lakini ndiye mfungaji mabao bora wao ambapo amewafungia mabao 42. Ndiye tegemeo lao kuu kwa mabao Urusi.
![Hernand Dario Gomez](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/81C0/production/_98261233_pancpachj.jpg)
Wachezaji wa Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja. Ni wachezaji watatu pekee wa kikosi chao huchezea soka Ulaya.
Meneja wao? Raia wao wa Colombia Hernan Dario Gomez amekuwa mkufunzi kimataifa kwa muda mrefu, ambapo amewaongoza Colombia mara mbili. Hii itakuwa mara yake ya pili kuongoza timu Kombe la Dunia baada ya kuwafikisha Colombia michuano ya 1998 ambapo walilazwa na England 2-0 kwenye Kundi G.
ASIA
Iran
Ustadi: Ni mara ya tano Iran kufuzu Kombe la Dunia.
Mechi pekee waliyoshinda ni 2-1 dhidi ya Marekani michuano ya Ufaransa '98.
![Carlos Queiroz](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/C1F8/production/_97665694_carlosqueiroz_getty.jpg)
Mchezaji nyota: Mshambuliaji Sardar Azmoun ambaye kimsingi ndiye mshambuliaji bora zaidi Asia baada ya raia mwenzake Ali Daei, ambaye amefunga mabao mengi kimataifa kuzidi mchezaji mwingine yeyote wa kiume. Azmoun, 22, ni stadi sana kwa miguu na kwa kichwa. Huchezea Rubin Kazan ya Urusi.
Wachezaji Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja
Mkufunzi? Carlos Queiroz amekuwa mkufunzi kwa muda mrefu na ana tawasifu ya kupendeza. Amukuwa mkufunzi Sporting Lisbon, Afrika Kusini, Real Madrid na alikuwa msaidi wa Sir Alex Ferguson Manchester United.
Na amehudumu mara mbili Ureno.
Amekuwa mkufunzi wa Iran kwa miaka sita iliyopita.
Japan
Ustadi: Wameshiriki tangu 1998, Japan na walipita hatua ya makundi mara mbili, ikiwa ni pamoja na 2002 walipokuwa wenyeji wenza na Korea Kusini.
Mchezaji nyota: Keisuke Honda, Shinji Kagawa na nyota wa Leicester Shinji Okazaki wamekuwa wachezaji nyota. Lakini kuna kinda wa Arsenal Takuma Asano ambaye tayari amefungia cnhi yake mechi tatu na alisaidia Stuttgart kupanda daraja Bundesliga msimu uliopita akiwa kwa mkono kutoka kwa Gunners. Wenger amemweleza kama mshambuliaji mwenye kipaji na mwenye matumaini siku za usoni.
Wachezaji Ligi ya Premia: Maya Yoshida (Southampton), Shinji Okazaki (Leicester City), Takuma Asano (Stuttgart, kwa mkopo kutoka Arsenal).
Mkufunzi? Vahid Halilhodzic, ingawa huenda akaondoka kwani kuna fununu kuhusu mzozo kwenye timu.
Aliongoza Algeria kufika hatua ya muondoano mara ya kwanza 2014.
Ni mchezaji wa zamani wa Yugoslavia ambaye amewahi kuwa mkufunzi wa Paris St-Germain, Dinamo Zagreb na Ivory Coast.
![Nasser Al Shamrani](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/15FAC/production/_97682009_saudi_arabia_getty.jpg)
Saudi Arabia
Ustadi: Saudi Arabia walishinda mechi zao pekee Kombe la Dunia mara yao ya kwanza 1994, waliposhinda mechi mbili za hatua ya makundi na kufika raundi ya pili.
Ushindi wao mechi ya pili, 1-0 dhidi ya Ubelgiji, ulitokana na moja ya mabao yanayokumbukwa zaidi - Saeed Al Owairan alipokimbia kutoka nusu yao ya uwanja na kuwachenga nusu ya walinzi wa Ubelgiji kisha kufunga.
Mchezaji nyota: Mshambuliaji mkongwe Nasser Al Shamrani atakuwa na mchango muhimu.
Ni mchezaji bora wa mwaka Asia mwaka 2014.
Wachezaji Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja
Mkufunzi? Bert van Marwijk, ambaye amekuwa kwenye usukani tangu 2015. Mholanzi huyo wa miaka 65, aliwaongoza Uholanzi kufika fainali Kombe la Dunia 2010. Amekuwa pia mkufunzi wa Borussia Dortmund, Feyenoord na Hamburg.
Korea Kusini
Ustadi:Ndiyo timu ya Asia yenye rekodi nzuri. Hufahamika kwa jina la utani Mashujaa wa Taegeuk. Walifuzu kwa michuano yao ya 10 kwa sare dhidi ya Uzbekistan. Urusi itakwua mara yao ya tisa mtawalia kushiriki.
![Lee Dong-gook will be 39 by the time the World Cup begins in Russia](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/138F6/production/_97681108_gook.jpg)
Mchezaji nyota: Son Heung-min alionyesha ustadi wake Tottenham. Hata hivyo, amefunga bao moja pekee kimataifa tangu 2016. Mfuatilie zaidi Lee Dong-gook aliyeingia kama nguvu mpya mechi yao ya mwisho ya kufuzu na ambaye atakuwa na miaka 39 michuano ikianza mwaka ujao. Ni mshambuliaji wa zamani wa Middlesbrough ambaye amechezea timu ya taifa mechi 105 miaka 19.
Wachezaji Ligi ya Premia: Ki Sung-yueng (Swansea), Son Heung-min (Tottenham)
Mkufunzi? Shin Tae-yong ambaye amepewa jina la utani 'Mourinho wa Asia' amekumbwa na shinikizo kutokana na kutofanikiwa sana mechi za kufuzu. Hata hivyo, alichukua usukani Julai na huenda akapewa muda zaidi. Ana miaka 48 na alicheza Ligi Kuu ya Korea Kusini miaka 12 na mechi moja ligi kuu Australia kabla ya kustaafu 2005.
AFRIKA
Misri
Ustadi: Misri wamo nafasi ya 30 orodha ya Fifa, moja chini ya Uholanzi. Hawakufuzu michuano ya 2010 na 2014 baada ya kushindwa mechi za muondoano za kufuzu baada ya hatua ya makundi.
Wamefuzu kwa bao la ushindi kutoka kwa Mohamed Salah wa Liverpool dhidi ya Congo 8 Oktoba.
Ufanisi wao mkubwa karibuni ni mwaka 2010 waliposhinda Kombe la Mataifa ya Afrika mara yao ya saba.
![Mohamed Salah has scored six goals in qualifying but has never been to a World Cup competition](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/C06E/production/_98226294_gettyimages-633365042.jpg)
Mchezaji nyota: Mohamed Salah, aliyenunuliwa na Liverpool majira ya joto, ndiye mchezaji mwenye kipaji zaidi Misri. Ana kasi sana na amefunga mabao 32 mechi 56 za kimataifa, zikiwemo tano mechi za kufuzu kwa Urusi.
Wachezaji Ligi ya Premia: Mohamed Salah (Liverpool), Mohamed Elneny (Arsenal), Ahmed Hegazy (West Brom), Ramadan Sobhi (Stoke),
Wachezaji Championship: Ahmed Elmohamady (Aston Villa)
Wachezaji League One: Sam Morsy (Wigan),
Mkufunzi? Raia wa Argentina Hector Cuper, ambaye amewahi kuwa mkufunzi waValencia na Inter Milan, alichaguliwa kuwa mkufunzi mkuu Machi 2015.
Alikuwa pia mkufunzi wa Georgia kati ya 2008 na 2009.
Michuano yake mikubwa kuongoza timu ilikuwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 ambapo Misri walilazwa 2-1 kwenye fainali na Cameroon.
Nigeria
Ustadi: Hii itakuwa mara ya sita kwa Nigeria kushiriki fainali za Kombe la Dunia, ma mara yao ya tatu mtawalia.
Wamefika hatua ya 16 bora mara tatu - 1994, 1998 na 2014 - lakini hawajawahi kupita hatua hiyo.
Mchezaji nyota: Nahodha wao John Mikel Obi, ndiye mchezaji wao mwenye uzoefu zaidi kikosini, ambapo amechezea taifa mechi 80 na atakuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Super Eagles Kombe la DUnia Urusi.
Itakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea kushiriki michuano hiyo.
Mikel, 30, aliwasaidia kufika hatua ya muondoano 2014 kwa mara ya kwanza tangu 1998.
Kwa sasa yeye huchezea klabu ya Tianjin Teda ya China.
![John Mikel Obi](https://ichef.bbci.co.uk/news/695/cpsprodpb/4F58/production/_98221302_hi041396527.jpg)
Wachezaji Ligi ya Premia: Alex Iwobi (Arsenal), Victor Moses (Chelsea), Kelechi Iheanacho (Leicester City), Wilfred Ndidi (Leicester City), Ahmed Musa (Leicester City) na Ola Aina (kwa mkopo Hull City kutoka Chelsea).
Mkufunzi? Gernot Rohr ambaye amefanya kazi ya ukufunzi nchi nyingi duniani ndiye mkufunzi wao kwa sasa.
Amewahi kuwa mkufunzi Nice hadi Gabon, Burkina Faso hadi Nigeria.
Mjerumani huyo wa miaka 64 ana tajriba ya hali ya juu.
Rohr alichezea Bayern Munich na Bordeaux.
Kisha alikuwa mkufunzi wa Bordeaux waliposhindwa fainali ya Kombe la Uefa mwaka 1996 na Bayern.
Klabu alizowahi kuwa mkufunzi ni pamoja na Nantes ya Ufaransa, Young Boys Berneya Uswizi, Etoile du Sahel na pia amewahi kuwa mkufunzi Niger.
Comments
Post a Comment