Kombe la Dunia 2018 - mambo muhimu kuhusu nchi ambazo tayari zimefuzu michuano ya Urusi 13 Oktoba 2017 Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar ndiye mchezaji ghali zaidi duniani Michuano ya mwisho ya hatua za makundi kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka ujao inaendelea kufanyika. Kwa sasa mataifa 22 tayari yamejikatia tiketi kushiriki michuano hiyo itakayoshirikisha nchi 32 mwaka ujao. Mabingwa mara tano Brazil wamefuzu, sawa na mabingwa watetezi Ujerumani, pamoja na Argentina, Iceland, Ubelgiji , Colombia, Costa Rica, England, Misri , Iran, Japan, Mexico, Nigeria, Panama, Poland, Saudi Arabia, Serbia, Korea Kusini , Ufaransa, Ureno, Uhispania na Uruguay . Wali...