SHERIA NA MAKOSA YA JINAI

ELIMU YA SHERIA KITAIFA
Tanzania huwa na siku ya sheria kitaifa, kwa mwaka huu siku hii inaadhimishwa tarehe 01/02/2018.
Kauli mbiu ya siku ya sheria ni "MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA UTOAJI HAKI KWA WAKATI ILI KUTOA MAADILI"

Jukumu la kutoa haki lipo chini ya mahakama
Matumiziya tehamana katika kutoa haki kwa wakati kunategemeana na Tekinologia  inavyokua kwa mfano matumizi ya KOMPYUTA.taarifa za kesi huingizwa kwenye kompyuta kwakuwa na vitu vyote muhimu vinavyohusu kesi

Kesi husikilizwa kwa miezi sita na taarifa zote huwekwa kwenye kompyuta. Kesi ikisikilizwa hutumwa kwa mtandao kupitia compyuta
Mahakama ya mwanzo inatakiwa kusikiliza kesi na kutolea maamuzi na kumaliza kesi hiyo kwa muda wa miezi sita, kwenye mahakama ya mkoa ni kwa mwaka mmoja. Aina hizi za mahakama zikishindwa kumaliza kesi zake kwa wakati zinahitajika ziwajibike( mahakimu ndio walengwa wa uwajibikaji)

MAKOSA YA JINAI
Mshitakiwa akikamatwa hupelekwa polisi na ndani ya masaa 24 lazima kesi yake isikilizwe mahakamani, zaidi ya hapo mshitakiwa anayo haki ya kuhoji kwa mkuu wa upelelezi ili kupata haki yake.
Makosa ya jinai kama vile uvamizi, uhujumu uchumi, na mauaji mshitakiwa hana haki ya mdhamana , lakini kwa makosa mengine kesi zinayo haki ya mdhamana na kumbuka Mdhamana ni bure hauhitaji malipo
Tuwekane sawa katika kipengele cha dhamana.
Dhamana ya polisi; siku mtuhumiwa anapelekwa mahakamani polisi huweza kumpa mdhamana wa kuondoka na kurudi kesho yake ni bure na haihitaji fedha.

JINSI YA KUTOA TAARIFA KWENYE NGAZI ZA JUU PALE UNAPO DHULUMIWA HAKI YAKO MAHAKAMANI
Ukifika mahakama yoyote kuna mabango yenye namba ambazo niza mamlaka ya juu zaidi au zenye nguvu zaid ya hakimu. Na unapopiga simu huenda moja kwa moja makao makuu yaliyopo mikoa ya mbali ambayo ukisema ni kwenda kwa namna ya kawaida hutoweza kufanikisha jambo lako kwa wakati. Hivyo tunaweza kuona ni jinsi gani tekinologia inavyo weza kutoa msaada wa haraka katika kupata haki yako
Kumbuka kuwa dhamana haizidi siku 60 ina maana kuwa na upelelezi utakua umekamilika hivyo kesi inatakiwa isikilizwe, ikitokea tofauti unayo haki ya kuhoji na kama utaona hakiyako inasua sua unaweza pia kuripoti tatizo lako makao makuu.

RUFAA
Tambua kuwa hakimu wa ngazi ya wilaya kwa mwaka anatakiwa asikilize kesi zisizo pungua 250. Na baada ya kesi na hukumu kutolewa kwa makosa ya jinai mtuhumiwa au mlalamikaji anatakiwa kusubiru kwa siku 31 ndipo awe na haki ya kupata form ya kukata rufaa.

KESI ZA MADAI
Kwa kesi za madai mlalamikaji anatakiwa kwenda mahakani na kulipa todho na kupewa stakabadhi nipo mambo mengine yaendelee, usikubali kutoa todho bila kuchukua stakabadhi na kama ukiona kusuasua kwa huduma kumbuka kupiga simu makao makuu.

KESI ZENYE CHANGAMOTO KUBWA
Madai ya mirathi
Kesi za miradhi ndizo zimekua changamoto kubwa sana katika jamii zetu zinazotuzunguka. Mirathi ni mali anazoacha mtu baada ya yeye kufariki hivyo zile mali zaweza kugawanywa kwa njia mbalimbali kutokana na vikao vitavyo kaliwa na wana ndugu na wanafamilia wa marehemu agenda kuu ikiwa ni kumpata mtu atakae kuwa msimamizi wa mirathi hiyo na kutambua hatima ya watoto wa marehemu, mtu huyo akipatikana yeye ndiye atakae gawa zile mali kulingana na huduma zinazo hitajika na mke au watoto wa marehemu. Ikumbukwe kuwa msimamizi wa mirathi anaweza kutoka nje ya familia au ndani ya familia au ukoo ikimaanisha kuwa msimamizi wa mirathi anaweza kuwa hata mke au mtoto wa marehemu cha muhimu ni kwamba awe kafikia umri wa utu uzima. Matatizo mengi ya mirathi yanatokea pale msimamizi anapokua hatendi haki katika ugawaji wa ile mirathi na pengine anaweza kujijali yeye zaidi ya wale walengwa haswa wa mali zile. Nini cha kufanya pale hali ya kudhulumiwa haki ya mirathi inapotokea?
Vitu  ya muhimu vya kuwa navyo wakati unakwenda mahakamani
Kuwa na nyaraka zifuatazo

  • vikao ambavyo wanandugu wamekaa
  • nyaraka ya kifo ( cheti cha kifo)
  • Kama ni mke bhasi kuwa na cheti cha ndoa ( hapa kwenye jambo la ndoa pia huwa panakua na tatizo. Ieleweke kuwa kuna aina nne za ndoa. 1. Ndoa za kitamaduni, 2. Ndoa za bomani, 3. Ndoa za kanisani au misikitini, 4. Ndoa za mahakamani. Katika aina hizi nne za ndoa za kitamaduni hazina cheti lakini zilizo baki huwa zinakua na cheti lakini hawa wanandoa wa ndoa za kitamaduni wakihitaji wanaweza kupata cheti cha ndoa yao kama wataenda mahakamani na kujisajili kwaajili ya kupata cheti cha ndoa yao).

 vitu hivyo viambatanishe kisha nenda mahakamani kufungua kesi. Lakini cha umuhimu kuelewa ni kuwa kesi itachukua siku 90 ili kusikilizwa kwasababu ya kupitisha matangazo ili kuthibitisha kama kuna mtu mwenye pingamizi la haki. Kama litatokea pingamizi na hakimu ataona linamashiko atarudisha kesi kwenye ngazi ya familia au ukoo ili wajadili zaidi hiyo mirathi.
Atakaye chaguliwa kama msimamizi wa mirathi atatakiwa kujaza form namba 4 ambayo ataipata mahakamani na kama marehemu ni mfanyakazi wa serikali ataenda nayo benki.
Pia kwenye kesi msimamizi wa mirathi anatakiwa aandae taarifa ya wategemezi wa mirathi kama watoto na mke wa marehemu
Zaidi soma hapa kujua zaidi
http://sheriatanzania.blogspot.com/2007/06/sheria-ya-mirathi-ya-tanzania.html

NYONGEZA
Kesi ya kugushi sahihi
Sheria kifungu cha 333 sura ya 6 inaelezea adhabu ya mtuhumiwa huyo kama ifuatavyo
Kwanza kabla ya hukumu au adhabu mshitakiwa apewe haki ya kuomboleza ili asipewe afhabu kali
Adhabu ya kugushi sahihi ni miaka mi tatu
Na ikiwa umepata faida kwaajili ya kugushi sahihi adhabu ni miaka 15.

REFERENCE

  • http://sheriatanzania.blogspot.com/2007/06/sheria-ya-mirathi-ya-tanzania.html
  • 31/1/ 2018 SEMINA

Comments

Popular posts from this blog