HABARI LEO


Mkurugenzi ataka TSN ibebe ajenda ya viwanda
MKURUGENZI wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbasi ameitaka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kueleza na kuufafanulia umma ajenda ya serikali kujenga uchumi wa viwanda.
Dk Abbasi alitoa msisitizo huo mjini Dodoma jana alipotembelea ofisi za TSN Dodoma na kukutana na wafanyakazi wa ofisi hiyo. Pamoja na mambo mengine, aliwataka wafanyakazi wa kampuni hiyo kujielewa kwamba wana wajibu mkubwa wa kuiandika ajenda ya serikali ya uchumi wa viwanda. Aliitaka TSN kuandika habari kwa kuzingatia maadili na weledi na zilizofanyiwa uchambuzi wa kina zaidi, kuelimisha umma malengo hayo ya uchumi wa viwanda.
Dk Abbasi alisema kama waandishi watadhamiria kuibeba ajenda ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda, lazima wasome na kuzielewa nyaraka mbalimbali za serikali, mpango wa maendeleo wa serikali wa miaka mitano na mipango iliyomo kwenye bajeti ili kuwajulisha Watanzania juhudi za serikali kujenga uchumi.
Dk Abbasi, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi TSN kuhusu matangazo, Dk Abbasi alisema inakusudia kuanzisha Wakala wa Serikali wa Matangazo (WSM) kukusanya matangazo kutoka wizara, taasisi na wakala wa serikali na kuyatangaza kadiri ya umuhimu. “Utafiti uliofanyika umebaini nchi zaidi ya 30 duniani zinatumia mtindo huo ambapo anakuwapo wakala wa matangazo ya serikali ambaye atakusanya na kusambaza kwenye vyombo na malipo atafuatilia yeye,” alisema.

Comments

Popular posts from this blog