BIASHARA ANAZOWEZA KUFANYA MWANACHUO PINDI YUPO CHUONI
BIASHARA ANAYOWEZA KUFANYA MTU PINDI YUPO SHULENI
Ni muda mwingine na wasaa mwingine ambao tuna kila sababu ya kumshukuru mwenyenzi Mungu kwa kutuweka salama na hai wenye nguvu hata kuweza kusoma makala hii inayo husu mambo ya kiuchumi na maisha mazuri ya kijana yeyote yule iwe anasoma au la lkn wote tutafaidikaBIASHARA NI NINI
Biashara ni kitu chochote mtu anaweza kufanya ili kujipatia kipato. Lakin kutokana na maisha kua magumu na pia ushindani uliopo kila mmoja akijitahidi kwa namna yake kujikwamua kiuchumi bhasi inabid kila mtu anapofanya biashara kuwa na umakin pia kutumia akili nyingi ili kuwashinda au kuwa mshindani bora kwenye soko la ujasiriamali
1. Ujasiriamali wa taarifa
Hii ni biashara ambayo unatoa taarifa mbalimbali ambazo zinaweza kuwasaidia watu na hatimaye wakawa tayari kukulipa au ukafaidika kwa njia nyingine. Kuanza biashara hii unachagua ni aina gani ya taarifa ambazo unapenda kufuatilia au kutoa kisha unaanzisha blog ambayo utakuwa unatoa taarifa hizo. Ukitoa taarifa nzuri utapata watembeleaji wengi na hatimaye unaweza kuwauzia bidhaa au huduma nyingine au kuuza nafasi za matangazo kwenye blog yako hiyo na ukapata kipato kizuri.
2. Biashara ya mtandao
Hii ni biashara ambayo mwanafunzi anaweza kuifanya kwa muda mchache kila siku au kila wiki na baada ya mwaka au miaka miwili akawa ametengeneza mafanikio makubwa. Hii ni biashara ambayo unatengeneza mtandao wa watumiaji wa bidhaa au huduma na hivyo wanaponunua biashaa au huduma hiyo wewe unalipwa kamisheni. Kuna makampuni mengi yanafanya biashara hii kwa hapa kwetu Tanzania, zifuatilie vizuri kampuni hizi na chagua ni ipi unayoweza kuingia na kufanya biashara. Mbali tu na kufanya biashara pia utajifunza biashara katika ulimwengu halisi.
TAMBUA KUWA; Ukiwauliza watu kuhusu biashara hii watakukatisha tamaa sana kwa sababu wengi wa waliofanya biashara hizi wameshindwa kwa sababu mbalimbali, wewe unaweza kama ukiamua na usipokata tamaa.
3. Fanya biashara inayohusiana na TEHAMA
Teknolojia ya habari na mawasiliano(IT & ICT) bado inakua kwa kasi sana. Kama unapenda kutumia kompyuta au mtandao unaweza kufanya biashara nzuri sana inayohusisha IT. Unaweza kujifunza vitu kama kutengeneza picha(graphic design), kutengeneza website, kutengeneza program za kompyuta na hata za simu(mobile app). Ukishajua kutengeneza vitu hivi na ukawa mbunifu unaweza kutengeneza biashara nzuri na kubwa sana.
4. Endeleza vipaji vyako.
mmoja wetu ana vipaji au vitu fulani anavyopendelea kufanya. Unaweza kutumia muda huu wa chuo kuendeleza vipaji vyako na kuangalia ni jinsi gani unaweza kuwafanya watu wakulipe kupitia kipaji chako, Unaweza kuwa na kipaji cha kuimba, kuigiza, mitindo, kuandika na kadhalika. Weka muda maalumu wa kuendeleza kipaji chako kila siku. Kwa mfano kwa wanaopenda kuandika nashauri utenge saa moja kila siku kwa ajili ya kuandika tu, kwa njia hii utaboresha uandishi wako.
5. Uchuuzi wa kawaida.
Unaweza pia kufanya biashara nyingine ndogo ndogo kwa maeneo ya chuoni au unakoishi. Angalia ni bidhaa au huduma gani wanafunzi wanazihitaji ila wanazikosa au hawazipati kwa kiwango kizuri kisha ingia kwenye biashara hiyo na toa huduma nzuri sana. Utatengeneza biashara nzuri na yenye faida.
Mtaji wa kuanzia unatoa wapi?
Hili ni swali ambalo baadhi wameshajiona kwamba hawawezi kufanya biashara hizo kwa sababu hawana mtaji. Biashara zote nilizozungumzia hapo zinaanza na mtaji kidogo sana na nyingine kama ujasiriamali wa taarifa unaweza kuanza bila hata ya mtaji ni wewe na kopmyuta yako tu. Lakini zile zinazohusisha mtaji kidogo unaweza kuupata kama ukijitoa na kujituma pia nitakuja kuandika jinsi ya kupata mtaji kwa wakati mwingine.
Hizo ndizo baadhi ya biashara ambazo mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kufanya. Kumbuka sio biashara hizo tu ndio zinawezekana, bali hizo ni chache ambazo nina uhakika zinawezekana. Hivyo kama una wazo lako jingine la biashara bado unaweza kulifanyia kazi.
Pia biashara hizo sio rahisi, ila kama umedhamiria kweli na ukajituma kweli inawezekana. Lakini kuwa makini na masomo yako biashara isikutawale zaidi ya masomo yako.
Na utakapoanza maisha hayo ya kusoma na kufanya biashara kuna vitu unatakiwa uache, baadhi ni, kuangalia tv, movie, mipira, kuperuzi mitandao muda wote n.k
NYONGEZA; Ushauri huu hapa unategemea hauwezi kuwa sawa kwa kila mtu na wewe kama mwanafunzi wa chuo kikuu unaweza kuangalia ni kipi kinaweza kufanya kazi kwako na kisha kukiboresha zaidi kulingana na mazingira uliyopo.
kila la kheri katika mafanikio ya masomo yako na biashara yako. God bless you
REFERENCE
- https://amkamtanzania.com/2014/10/27/ushauri-biashara-ambazo-mwanafunzi-wa-chuo-kikuu-anaweza-kufanya-bila-kuathiri-masomo-yake/
Usisahau kusubscribe
Comments
Post a Comment