Tetesi za soka Ulaya Jumatano 10.10.2018: Mourinho, De Gea, Conte, Sancho, Henry, Terry

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 10.10.2018: Mourinho, De Gea, Conte, Sancho, Henry, Terry

MourinhoHaki miliki ya pichaPA
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho atafanya mazungumzo na Mkurugenzi wa timu hiyo Ed Woodward jijini London kabla ya bodi ya klabu kufanya mkutano wake siku ya Alhamis. (Sun)
United imeendelea kuwa na imani kuhusu mkataba wa mlinda mlango David de Gea ingawa amekuwa akihusishwa kuihama timu hiyo mara kadhaa, De Gea 27, amekuwa kwenye mazungumzo na Manchester juu ya mkataba mpya. (ESPN)
Antonio ConteHaki miliki ya pichaREUTERS
Chelsea inafanya mazungumzo na Antonio Conte kumumalizia malipo ya malimbikizo yake huku kukiwa na taarifa ya kumuandaa kurudi Chelsea, ingawa amekuwa akihusishwa na kujiunga na Manchester United, Real Madrid na Bayern Munich. (Telegraph)
Monaco imeanza kufanya mazungumzo na mshambulaiji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry, 41,kuwa mbadala wa Jardim. (Sun)
Thiery HenryHaki miliki ya pichaREUTERS
Beki wa Chelsea na timu ya taifa ya England John Terry ameongeza uwezekano wa kuwa kocha wa Aston Villa baada ya Monaco kuingia katika rada za Henry kuwa kocha wao. (Times)
Wachezaji wa Aston Villa wamependekeza jina la John Terry, 37, kuwa kocha wao baada ya kukiongoza kikosi hicho kama Nahodha mkuu alipokuwa anacheza kwenye ligi daraja la kwanza. (Mirror)
Klabu ya Manchester City itakuwa kwenye nafasi nzuri ya kumsanii kwa mara ya pili kinda wa England Jadon Sancho, 18, anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund baada ya kuonyesha nia ya kumsajili ingawa itatakiwa kutumia pesa kubwa.(Manchester Evening News)
Tottenham imepanga kumsajili kiungo kutoka Lyon na Ufaransa Tanguy Ndombele, 21, katika dirisha dogo la usajili mwezi wa Januari. (Mirror)
Beki wa kushoto wa Liverpool Moreno, 26, amewekwa kwenye mikakati ya Barcelona kama mubadala Jordi Alba. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Maneja wa Manchester United Jose Mourinho amepanga kumfuatilia mwenyewe kwa lengo la kumsajili beki wa Fiorentina na Serbia, Nikola Milenkovic, 20, (Telegraf, via Talksport)
Golikipa wa Stoke England Jack Butland, 25, ameachana na wakala wake wa mda mrefu jambo ambalo linaweza kumshuhudia kurejea kwake katika ligi kuu England. (Telegraph)
Manchester City imepanga kuanza mazungumzo na winga wa Ujerumani Leroy Sane, 22, kumshawishi aongeze mkataba mpya. (Sun)
Wakala wa Christian Eriksen amesema kuwa taarifa zinazosambaa kuwa mwajiri wake anasumbuliwa na maumivu makali ya tumbo sio za kweli ingawa anasumbuliwa kwa hivi sasa. (London Evening Standard)
Klabu ya Manchester United usajili wa dirisha dogo unaweza usifanikiwe sana kutokana na uwezekano wa kuathirika na Brexit, maneno haya aliyasema Profesa mmoja wa michezo. (Manchester Evening News)
Mshambulaiji wa Argentina Mauro Icardi hajaanza bado mazungumzo ya kupata mkataba mpya na klabu yake ya Inter Milan ingawa bado ana mkataba na klabu hiyo, mshambuliaji huyo anaweza kutolewa Milan kwa dau la pauni milioni 96. (Tiki Taka, via Goal)
Mauricio Pochettino
Kocha mkuu wa Tottenham Mauricio Pochettino na Kocha wa Arsenal Unai Emery wameweka utofauti wao pembeni na kusoma pamoja mafunzo yanayotolewa na Uefa. (Mail)
Beki wa kulia wa Tottenham Danny Rose, 28, amemtetea mchezaji mweza Harry Winks, 22 baada ya kuwepo kwa madai ya kushuka kiwango kwa winga huyo kunachagizwa na kupewa sifa ya kucheza kama Inesta. (London Evening Standard)

Comments

Popular posts from this blog