Watanzania wasikitishwa na kifo cha mtoto wa Muna Love, Patrick Dickson Tanzania 4 Julai 2018 Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha @PATDASMARTBOY Image caption Patrick anakumbukwa kwa utanashati wake namna alivyokua akivaa na kupendeza Mtoto wa msanii wa Filamu za Bongo na Mjasiriamali, Rose Alphonce maarufu kama 'Muna Love' ameaga Dunia. Mtoto Patrick Dickson ambaye alikua na umaarufu sana katika mitandao ya kijamii amefariki jana Julai 3, 2018 nchini Kenya alipokuwa akipatiwa matibabu. Baba aliyemnyonyesha mtoto wake mchanga wakati mama hakuweza Jitihada za kutafuta mabaki ya marubani wa Marekani wa Vita vya Pili vya Dunia Patrick alianza kuugua tangu mwaka 2016, ambapo alisumbuliwa zaidi na maradhi ya mguu hali iliyo mpelekea kushindwa kutembea. Kuanzia hapo Patriki alilazwa na kufanyiwa upasuaji mara kad...