Kombe la Dunia 2018: Ufaransa mabingwa wa dunia baada ya kuwacharaza Croatia 4-2, Mbappe na Pogba wafunga
Kombe la Dunia 2018: Ufaransa mabingwa wa dunia baada ya kuwacharaza Croatia 4-2, Mbappe na Pogba wafunga Saa moja iliyopita Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Ufaransa washinda Kombe la Dunia 2018 baada ya kuwacharaza Croatia 4-2 katika fainali iliyochezewa Urusi. Ufaransa iliyoingia mechi hiyo ikisaka ubingwa wa dunia kwa mara ya pili tangu 1998, ilitangulia kwenye mechi na goli la kwanza dakika ya 18 kufuatia mkwaju wa Antoine Griezmann ulioelekezwa wavuni na Mario Mandzukic. Mandzukic, shujaa dhidi ya Uingereza nusu fainali kwa kuipa goli la ushindi muda wa ziada, alimiminiwa lawama kwa kujifunga na kuwa mchezaji wa kwanza kupiga mpira hadi lango lake katika fainali ya Kombe la Dunia. Uongozi wa Ufaransa ulidumu kwa dakika 10 pekee kwani winga matata wa Croatia anayeichezea Inter Milan Ivan Peri...