Rais Magufuli asema hatochoka kubadili mawaziri 12 Novemba 2018 Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha IKULU Rais wa Tanzania John Pombe Magfuli amesema hatachoka kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri kila itakapohitajika. Ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake, tayari Magufuli ameshafukuza kazi mawaziri tisa kati ya 19 aliowateua Desemba 10, 2015. Akizungumza leo Ikulu katika hafla ya kuwaapisha mawaziri wapya, Rais Magufuli amesema ataendelea kufanya mabadiliko ya baraza lae pale patakapokuwa na uhitaji wa kufanya hivyo. "…hii ni kama safari, sio lazima wote tufike. Inawezekana hata mie kiongozi nisisfike lakini lengo letu lazima litimie," amesema Magufuli. Serikali 'yakaza buti' mzozo wa korosho Tanzania Korosho zaondoka na mawaziri wawili Tanzania Korosho zageuka kaa la moto Tanzania Mawaziri wapya...